Posts

Faida za unywaji wa maji yaliyochanganywa na ndimu kila asubuhi

Image
Umesikia mara nyingi kuwa kunywa maji kwa wingi hasa asubuhi kuna faida kubwa sana za kiafya mwilini,lakini kunywa maji yenye ndimu na vuguvugu kuna faida maradufu na ni rahisi kufanya kila siku. Vitamin C nyingi iliyomo katika limao na ndimu ni siri ya faida za tunda hili,ukiachia vitamini C ndimu ina vitamini B-complex,  madini ya Kalsiamu, chuma, magnesiamu na potasiumu, na fiba (Ndimu ina potasiumu kwa wingi kuliko tofaa(apple) au  Zabibu).  Kunywa maji peke yake (yasiyo na kitu) wakati wa asubuhi huwapa tabu baadhi ya watu,wengine hupata kichefuchefu . Lakini maji yaliyotiwa ndimu kidogo huwa na radha nzuri zaidi na watu wote wanaweza kunywa bila shida.  Kuna faida nyingi ambazo utazipata kwa kunywa maji yenye ndimu au limao na katika makala hii tunazitaja faida 11 muhimu.  Faida 11 za Kunywa Maji Yenye Ndimu  Faida #1: Huchochea Mmeng’enyo wa Chakula Tumboni  Maji yenye ndimu husaidia chakula kusagika vizuri na haraka katika mfumo wa chakula. Jap...

Ufahamu undani wa maumivu ya korodani

Image
Kuna wakati mwanaume huweza kupata maumivu ya korodani, ambapo inawezekana ikawa ni maumivu kwa korodani moja au zote mbili. Maumivu hayo yanaweza kutokea endapo korodani zitakuwa zimeumizwa au kupata maambukizi. Aidha, maambukizi hayo huweza kuwa makali na ya muda mfupi au makali kwa muda fulani halafu yanapoa yenyewe, lakini pia huweza kuwa ni maumivu ambayo siyo makali ila ni ya muda mrefu na yanayomnyima raha mhusika. Mbali na hayo, pia maumivu ya korodani huweza kuwa makali kiasi kwamba yatahitajika matibabu ya dharura mfano korodani inavimba kama jipu kubwa, ikiambatana na maumivu makali na homa, tatizo hili kitaalam huitwa ‘Fournier’s gangrene’. Kuna wakati mhusika anaweza kupata maumivu ya korodani mara inapotokea korodani ikajinyonga yenyewe na kusababisha mhusika kupata maumivu makali ya ghafla yanayoelekea hadi tumboni. Kimsingi maumivu ya korodani huchangiwa na vyanzo mbalimbali, lakini maumivu sugu ni yale yanayochukua takribani zaidi ya miezi mitatu. Vilevile ...

Faida Za Ulaji Wa Ndizi Kwa Wanaume Mlio Kwenye Ndoa

Image
Ndizi ni tunda linalopendwa na watu wengi sana kwenye jamii ya watanzania lakini je unajua ndizi zinaweza kukusaidia mwanaume kwenye shughuli za ndoa na kutimiza majukumu yako ya uwamaume vizuri kwa mke wako au mwenzi wako leo tutazame faida tatu za ndizi kwa wamaume kwenye sehemu ya mahusiano 1.Ndizi Ni Chanzo Kikubwa Cha Nguvu Mwilini Ndizi mbivu zina kiwango kizuri cha Glucose ambayo huingia kwenye damu moja kwa moja na kuleta msisimuko na kuongeza utendaji wa kazi wa mwilini si unasikia wachezaji wanaambiwa wabugie Glucose kwenye kipindi cha mapunziko sasa ndizi ni glucose salama zaidi tena sio glucose pekee na faida zingine kibao 2.Ndizi ina madini kiasi kikubwa ya Potassium  siku kuwa ukiwa na kisukari (BP) uwezo wako wa kucheza mechi kitandani unakuwa mdogo basi ndizi ina madini ya potassium ambayo yanasaidia kurekebisha kiwango cha sukari mwilini ndugu yangu kama ukila ndizi mbivu mbili kwa siku unadhani hiyo sukari inashushwa kiasi gani Stuka bwana 3.Ndizi husaidia Mfumo w...

Sababu zinazopelekea mtu kukoroma ukiwa umelala na jinsi ya kuzuia hali hiyo.

Image
Kukoroma ni tatizo linalowapata watu wengi wakati wanapolala ambalo linaweza kuwatokea watu wa kila umri ingawa hutokea mara nyingi kwa wanaume au watu wanene. Kukoroma kwa kawaida sio tatizo kubwa na mara nyingi huleta tu karaha kwa mtu anayelala karibu na mkoromaji. Mtu huwa anakoroma pale kunapokuwa na kitu au sababu yoyote itakayoziba kuingia au kutoka kwa hewa mdomoni na katika pua. Kuta za koo hutikisika wakati wa kupumua na matokeo yake ni sauti inayosikika ya kukoroma. Kuingia au kutoka kwa hewa huweza kuzuiwa na sababu mbalimbali kama vile. Kuziba tundu za pua kusiko kamili ambako husababisha nguvu zaidi zitumike katika kupitisha hewa kwenye pua wakati mtu akiwa amelala. Kitendo hicho hupelekea nyama laini za pua na koo zijikusanye na kusababisha mkoromo. Kuna baadhi ya watu wanakoroma tu kipindi cha allergy (allergy season) au wanapatwa na matatizo ya sinus. Baadhi ya matatizo kama vile kupinda pua (deviated septum) au ukuta unaotenganisha tundu za pua na polyps za pua pia hu...

Aina 10 za vyakula vinavyoweza kuondoa tatizo la upungufu wa nguvu za kiume

Image
Tatizo la uwezo wa kufanya tendo la ndoa linazidi kukua miongoni wa wanandoa na wapenzi wengi. Takwimu za kitafiti zinaonyesha kuwa karibu ndoa 4 kati ya 10 zenye umri wa miaka 3 na kuendelea zinakabiliana na tatizo hili. Aidha wanaume 6 kati ya 10 wanatajwa kulalamikia upungufu wa nguvu za kiume na kuacha idadi ya wanawake wanaokabiliwa na tatizo hilo kwa mujibu wa uchunguzi kubaki na asilimia 13. Pamoja na matatizo mengine kutajwa kuchangia upungufu wa nguvu za kiume na kushuka kwa msisimko wa tendo miongoni mwa wanandoa, uchunguzi umeonesha kuwa utumiaji holela wa vyakula hasa vyenye mafuta ni moja kati ya sababu zinazochangia kwa kasi tatizo hili. Kwa kuzingatia hilo, watafiti wa masuala ya uhusiano wa kimapenzi wamebaini aina kumi ya vyakula ambavyo vina uwezo wa kumuongezea mtu nguvu ya kufanya tendo la ndoa.Vyakula hivyo ni hivi vifuatavyo:- 1. PILIPILI Pilipili zilizocheshwa zimetajwa kuwa na uwezo wa kusaidia msukumo wa usambazaji damu mwilini, ambao kwa kiasi kikubwa ndiyo un...

Dalili za mwanamke mjamzito

Image
MWANAMKE anapopata ujauzito kwa kawaida huwa anaanza kuona dalili ambazo si za kawaida. Na ni wakati huo ambao ni muafaka kwake kuanza kuuchunguza mwili wake. “Homoni zinazosambaa mwilini mara tu unapopata ujauzito husababisha mabadiliko kadhaa katika mwili wake ambayo yanaweza kugundulika kabla hata ya uchunguzi halisi wa kujua kama mjauzito au la,” anasema Melissa Goist, Profesa na Mtalaama wa Masuala ya Uzazi wa Chuo Kikuu cha Ohio, Marekani. Maumivu kwenye matiti Hii ni dalili ya kawaida ya ujauzito ambapo nguvu za homoni mwilini huongezeka wakati yai linavyopata “rutuba”, jambo ambalo huongeza wingi wa damu na kuyafanya matiti ya mwanamke kuvimba na kuwa makubwa isivyo kawaida. Maumivu mwilini Utaanza kusikia maumivu kama vile unataka kuingia katika siku zako. Kwa kawaida hali hii hutokea wakati yai likiwa linasafiri kwenda katika chumba cha mimba. Hivyo, hali hiyo husababisha sehemu hiyo itanuke taratibu na kusababisha maumivu hayo. Kutokwa damu bila kutegemea "Wanawake weng...

Yatambue madhara ya kunywa pombe wakati wa ujauzito

Image
Matumizi ya pombe wakati wa ujauzito ni moja ya njia ya kuzuia kupata matatizo ya kuzaliwa nayo na udhaifu kwa mtoto. Pia kuna matatizo kadhaa yanaweza kutokea kwa kichaga kutokana na matumizi ya pombe wakati wa ujauzito . Madhara haya ya pombe huweza kuwa ya kujitambua tabia na madhara madhara ya mkusanyiko wa dalili na viashiria kwa mtoto vinavyoitwa fetal alcohol syndrome-FAS. Kutokana na shirika madhara ya pombe yanayoambatana na dalili na viashiria Fulani yanaongezeka sana. Pombe imekuwa ikituiwa vibaya sana wakati wa ujauzito ukilinganisha na madawa mengine. Dalili za mtoto ambaye mama alikuwa akitumia pombe kwa kiasi kikubwa Kutokuwa vema kabla na baada ya kuzaliwa Mtindio wa ubongo Udhaifu wa kuzaliwa wa kichwa na uso Magonjwa ya moyo Tabia zisizoeleweka Matatizo ya mfumo wa fahamu Kuhusu fetal alcohol syndrome Kiwango kikubwa cha pombe kwenye damu ya mama kipindi cha ujauzito huweza kuwa na uharibifu kwa kichanga akiwa tumboni na maendeleo ya mtoto baada ya kuzaliwa. Baadhi ya...