Sababu ya Mimba Kuharibika, Dalili na Matibabu yake Unapoona Dalili

Mimba kuharibika au kutoka ni hali ya mimba yenye wiki 28 au chini ya hapo kuharibika au kutoka. Hali hujulikana kama miscarriage au spontaneous abortion kwa kiingereza. Mtoto aliye tumboni katika umri huu hataweza kuishi nje ya tumbo la mama. Katika nchi zilizoendelea huchukuliwa mimba iliyo chini ya kipindi cha wiki 24. Zaidi ya asilimia 80 ya mimba huharibika katika miezi 3 ya kwanza ya ujauzito. Baada ya miezi hii kupita, uwezekano wa mimba kuharibika hupungua. Dalili Za Mimba Kuharibika Karibu asilimia 50 ya mimba zote huharibika hata kabla ya mwanamke kujua kama ni mjamzito, hasa ikisababishwa na matatizo katika vinasaba vya mtoto (congenital chromosomal abnormalities). Kwa mimba zilizoanza kukua dalili za mimba kutoka huwa ni Kutokwa Damu Kwenye Uke. Damu inaweza kutoka kama matone kwenye nguo za ndani na baadae damu nyingi, au damu nyingi kama ya hedhi.Maumivu ya Tumbo. Mara nyingi hutokea chini ya kitovu. Yanaweza kuwa makali sana.Kutoa tishu, mabonge ya damu na mabaki ya kiin...