Vyakula Vitakavyosaidia Kuilinda Afya ya Figo yako..!!!
Afya ya figo ni muhimu kama ilivyo afya ya moyo, hii ni kwa sababu figo ni moja ya kiungo ambacho husaidia kuchuja sumu mbalimbali ndani ya mwili na baadaye kutoa taka mwili kwa njia ya haja ndogo (mkojo) Matatizo ya figo huweza kuchangia ugumu wa upatikanaji wa haja ndogo (mkojo) au miguu na mikono kuvimba. Pia mtu mwenye shida ya figo huwa katika hatari kubwa ya kukumbwa na matatizo ya moyo. Ulaji unaofaa mara zote husaidia sana kulinda afya ya viungo vyote muhimu ndani ya mwili ikiwa ni pamoja na figo na kuifanya iweze kufanya kazi zake vizuri ndani ya mwili. Hata hivyo, kuna baadhi ya vyakula ambavyo tunaweza kusema ni vyakula rafiki kwa afya ya figo ndani ya mwili ni vyema ukafahamu hapa leo. Karibu>>> Kabeji, hii ni mboga ambayo wengi wetu tunaifahamu sana na tumekuwa tukiitumia katika maisha yetu ya kila siku, lakini ni vyema msomaji wangu ukatambua kwamba mboga hii nayo inauwezo mzuri wa kulinda afya ya figo yako. Samaki pia ni muhimu sana kwa afya ya figo, hii ni kwa ...