Jifunze namna ya kulainisha viganja au mikono
Moja ya hasara ya mwanamke aliye hodari na kazi za nyumbani ni viganja vya mikono kuwa vigumu au vikavu. 🎀Kama unafua na maji na sabuni, kuosha vyombo, kusafisha nyumba, kubadili watoto nepi au diapers,kupika n.k . usishangae kuwa na viganja vigumu au vikavu. 🎀Hakuna haja ya kuogopa na toa wasiwasi hii ni aina ya kufanya mikono yako iwe laini na ya kuvutia.
_ 🎀Huna haja ya kwenda kwa spa’s wala kwa wataalamu. Baada ya kazi zako fanya haya; 🕸Kunywa maji kwa wingi na kisha tumia njia hizi zifuatazo; 🕸Chukua container weka chumvi kiasi. 🕸Weka olive oil ndani ya container.
_ 🕸Weka sabuni ya maji ya kuoshea mikono, tumia aina unayoipenda inaweza kuwa anti-bacterial au yoyote ya maji. Ni vizuri kutumia sabuni ya maji, sababu ya kawaida hautaosheka vizuri mkono sababu maji na mafuta hayachanganyiki.
_ 🕸Kausha mikono yako vizuri, kisha weka mchanganyiko huo kwenye viganja vyako kiasi cha ½ kijiko cha chai kisha sugua pole pole. Sugua ndani na nje ya viganja na ndani ya vidole na kucha. 🕸Osha kwa maji ya uvuguvugu .
Kausha mikono kwa kutumia taulo kavu.
Pakaa lotion ya mikono .
_ 🎀AU🎀 🕸Osha mikono na maji ya uvuguvugu na sabuni kuondoa grease na bacteria. 🕸kisha kausha na taulo kavu.
Chukua sukari vijiko viwili(2) vya chai na olive oil pia vijiko viwili(2). Pakaa mikononi kwa pamoja haraka .
Sugua mikono yote kwa pamoja ndani na nje kwa kutumia mchanganyiko huo. 🕸Osha mikono kwa maji ya uvuguvugu. 🕸Tumia rose water pia nzuri . 🕸Kisha pakaa lotion ya mkononi. 🎀Waweza tumia pia sunflower oil na hata mafuta ya nazi pia mazuri.
_ 🎀TIPS🎀 🎀Usifanye mara moja ukategemea matokeo ya kudumu au milele. 🎀Tumia baby oil au lotion kabla ya kulala. 🎀Tumia lotion zinazotengenezewa na mimea zaidi. 🎀Acha lotion kwa dakika kumi(10)kwenye viganja,ile layer ya juu ya ngozi itanyonya lotion na italoki moisture ndani ya ngozi.Fanya hivi mara mbili(2) kwa wiki.
_ 🎀Vaa gloves au plastic wakati unafanya kazi kama kuosha vyombo au gardening .
Comments
Post a Comment